Mwinjuma: Tuendeleze vipaji vya watoto ili kujenga kizazi chenye uwezo wa kushindana kimataifa
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma, amewataka walimu, wazazi na wadau wa michezo kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuibua na kuendeleza vipaji vya watoto ili kujenga kizazi chenye uwezo wa kushindana katika medani mbalimbali za michezo kimataifa.
Mhe. Mwinjuma amesema hayo leo wakati akifunga Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Tanzania kwa Shule za Msingi ( UMITASHUMTA) mwaka 2026 yaliyofanyika mkoani Iringa.
Amesema kuwa, Serikali inatambua umuhimu wa Michezo kama burudani na nyenzo muhimu ya muhimu ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi na hivyo kuendelea kuwekeza kwenye miundombinu ya Michezo.
"Serikali inaamini michezo si burudani pekee, bali ni nyenzo muhimu ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Ndiyo maana tutaendelea kuwekeza katika miundombinu ya michezo, kuendeleza mashindano mbalimbali na kuhakikisha vipaji vya vijana vinatambuliwa na kuendelezwa,” amesema Mhe. Mwinjuma.
Aidha, ameeleza kuwa Mashindano mbalimbali yataendelea sambamba na kuhakikisha vipaji vya vijana vinaendelezwa.





Post a Comment