JUDE AIKATAA TUZO YA MAN OF THE MATCH
Kiungo wa timu ya Taifa ya England, Jude Bellingham amesema hakustahili kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mechi ya timu yake dhidi ya Ghana.
Mara baada ya mchezo huo wa Kombe la Dunia uliochezwa katika Jimbo la Massachusetts, Marekani, Bellingham alitangazwa kuwa Mchezaji Bora wa Mechi, tuzo ambayo nyota huyo wa England anaamini kwamba ilipaswa kwenda kwa mchezaji mmojawapo wa Ghana."Nilikuwa na nyakati kadhaa. Ilikuwa ngumu kuwa mchezoni na namshukuru kila aliyenipigia kura lakini ilipaswa kwenda kwa wale waliojilinda vyema, hivyo pongezi kwao", amesema Bellingham na kuongeza kuwa "Nadhani walikuja kucheza kwa ajili ya kutafuta sare kama ambavyo ilionekana na pongezi kwao kwa vile wamepata sare".
Katika mchezo huo, England ilionekana kuwa bora katika kumiliki mpira, kutengeneza nafasi na kulishambulia mara kwa mara lango la Ghana lakini haikufanikiwa kutikisa nyavu.

Post a Comment