CHALAMILA AWAITA WANANCHI SABASABA



Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kutembelea Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yanayofanyika katika Viwanja vya Julius Nyerere, Dar es Salaam.


Akizungumza na waandishi wa habari katika Viwanja vya Sabasaba, Chalamila amesema maonesho ya Sabasaba ni fursa muhimu kwa wananchi, wafanyabiashara na wawekezaji kujifunza kuhusu bidhaa, huduma na teknolojia mbalimbali zinazochochea maendeleo ya kiuchumi nchini.

Amesema maonesho hayo ya mwaka huu yana upekee mkubwa kutokana na kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwake, hatua inayoonyesha mchango wake katika kukuza biashara na uwekezaji nchini.

Aidha, amewataka wananchi kutumia fursa hiyo kujitokeza kwa wingi, kushiriki kikamilifu na kunufaika na fursa mbalimbali zinazotolewa na washiriki wa ndani na nje ya nchi.

Maonesho hayo yanatarajiwa kuanza Juni 28,2026.

No comments