NJOMBE SHAMBA LA FEDHA, WAKULIMA WA PARACHICHI WAVUNA BILIONI 49
Mkoa wa
Njombe umezidi kudhihirisha umahiri wake katika sekta ya kilimo ambapo katika
msimu wa mwaka 2024/25, wakulima wa zao la parachichi wamefanikiwa kujipatia
mapato ya jumla ya takribani shilingi bilioni 49.236 kupitia mauzo ya moja kwa
moja
Kati ya fedha
hizo, kiasi cha shilingi bilioni 31.2 zilitokana na tani 18,378.99 zilizouzwa
nje ya nchi kwa bei ya wastani wa shilingi 1,700 kwa kilo, huku tani nyingine
29,986.77 zikiuzwa kwenye viwanda vya ndani ya mkoa kwa wastani wa shilingi 600
kwa kilo na kuingiza shilingi bilioni 17.9
Takwimu
hizo zimetolewa na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa wakati akizungumza na
waandishi wa habari mkoani Njombe.
Alisema mafanikio
haya yanachangiwa na uwepo wa viwanda vitano vya kuchakata parachichi vikiwemo
AvoAfrica na Avodemia, vyenye uwezo wa kusaga tani 1,650 kwa siku, pamoja na
vituo tisa vya kufungashia ambavyo vinahudumia pia mikoa jirani ya Mbeya,
Iringa, Ruvuma, na Songwe
Pia wakati akielezea mafanikio ya
kilimo cha parachichi Msemaji wa
Serikali alimtambulisha mkulima mwenye ekari 200 za zao hilo, aliyemtambulisha
kwa jina moja la Msuya ambaye mwaka jana alifanikiwa kuuza matunda yake kwa Sh
3,700 kwa kilo kutokana na ubora wake. Wastani Wa mkoa kilo ni sh 1,700.
Alisema kwamba anapuzungumza
kilimo kinalipa huyo ni mfano mojawapo kwani kutokana na kilimo chake cha
kisasa aliweza kuvuna tani 200 alizopeleka sokoni kwa bei hiyo.
Amesema Serikali
kupitia Mfuko wa Dhamana wa Wakulima Wadogo na Benki ya Kilimo (TADB), imekuwa
ikichagiza uwekezaji huu ambapo hadi sasa TADB imetoa mikopo ya thamani ya
shilingi bilioni 173.11 katika kanda ya Nyanda za Juu Kusini kwa ajili ya
kuimarisha mnyororo wa thamani wa mazao kama parachichi na viazi

Post a Comment