TANZANITE QUEENS NDANI YA KUNDI LA KIFO KOMBE LA DUNIA
TIMU ya Taifa ya soka ya wanawake chini ya umri wa miaka 20 ‘Tanzanite Queens’ imepangwa Kundi B pamoja na Brazil, Canada na England katika fainali za Kombe la Dunia zitafanyika nchini Poland kuanzia Septemba 5 hadi 27 mwaka huu.
Katika droo iliyochezwa kwenye mji wa Łódź jana Kundi A lina wenyeji Poland, Korea Kusini, Argentina, Italia, KundI C ni Japan, Marekani, Ghana, Ecuador, Kundi D ni Hispania, Mexico, New Zealand, Benin, Kundi E ni Korea Kaskazini, Colombia, Costa Rica, Ureno na Kundi F ni Ufaransa, Nigeria, China, New Caledonia.
Mashindano hayo yanashirikisha jumla ya timu 24, zikiwemo timu nne kutoka Afrika ambapo Tanzania ‘Tanzanite Queens’ Nigeria, Ghana na Benin.
Fainali zitachezwa katika miji minne ambayo ni Bielsko-Biała, Katowice, Łódź, na Sosnowiec na bingwa mtetezi ni Korea Kaskazini baada ya kutwaa ubingwa huo nchini Colombia mwaka 2024

Post a Comment