Coca-Cola yaisitisha uzalishaji
Kampuni ya Coca-Cola imetangaza kusitisha kwa muda uzalishaji wa bidhaa zake za maziwa za Fairlife nchini Marekani kufuatia shambulio la ransomware katika mifumo yake ya uzalishaji.
Kampuni hiyo ilithibitisha tukio Alhamisi Julai 16, 2026 kupitia taarifa yake rasmi.
Taartifa hiyo imesema kubwa imebaini uwepo wa watu wasiohusika ambao wameingilia sehemu ya mifumo yake ya uzalishaj na wamelazimika kusitisha uzalishaji wa bidhaa hizo. Hata hivyo, shughuli zake za uzalishaji nchini Canada bado zinaendelea kama kawaida na hazijaathiriwa na shambulio hilo.
Kuhusu kiwango cha uharibifu uliotokea, Coca-Cola ilieleza katika taarifa yake iliyowasilishwa kwa Tume ya Usalama nchini Marekani kwamba hadi sasa bado hawajajua ukubwa kamili wa tatizo, asili, na athari za tukio hilo.
Kampuni hiyo ilisema kuwa kwa sababu hiyo, bado hawajaweza kubaini kama tukio hilo lina uwezekano wa kuathiri kwa kiasi kikubwa utendaji wa kampuni hiyo kwa ujumla.
Bidhaa ya Fairlife, ambayo inajulikana kwa mchakato wake maalum wa kuchuja maziwa ili kuongeza protini na kupunguza sukari, imekuwa bidhaa muhimu yenye thamani ya mabilioni ya dola kwa kampuni ya Coca-Cola.

Post a Comment