RAIS SAMIA AMPA PROF JAY MILIONI 30


Nguli wa muziki wa Hip Hop nchini na mbunge wa zamani wa jimbo la Mikumi, Joseph Haule maarufu kama Prof Jay, amepokea msaada wa Shilingi milioni 30 kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ikiwa ni sehemu ya kumwezesha kuendelea na maisha yake baada ya kutoka kwenye changamoto ya afya iliyokuwa ikimkabili.

Fedha hizo zilikabidhiwa Jana mei 10 2026 na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma, aliyemtembelea Prof Jay akiwa ameambatana na Mstahiki Meya wa jiji la Dar es salaam Nurdin Bilal Juma (Shetta).

Katika ziara hiyo, ujumbe huo ulimfikishia Prof Jay salamu maalum kutoka kwa Rais Samia, huku ukieleza kuwa Serikali inaendelea kuthamini mchango wake mkubwa katika tasnia ya muziki na jamii kwa ujumla.

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, Prof Jay amemshukuru Rais Samia kwa moyo wake wa upendo na namna alivyoendelea kumuunga mkono tangu alipokuwa akisumbuliwa na maradhi hadi aliporejea katika hali yake aidha amewashukuru Watanzania waliokuwa wakimuombea na kumpa faraja katika kipindi chote cha changamoto alizopitia.

No comments