SPACK KUZIKWA CHAMAZI KWA MKONGO KESHO
Aliyekuwa msanii wa Bongo Fleva, Selemani Mvamba almaarufu 'Spack', anatarajiwa kuzikwa kesho Aprili 28 Chamazi kwa Mkongo.
Meneja wa msanii huyo Abdulrahman Hassan almaarufu Malefti amesema msiba wa Spack ambaye alikuwa anaishi Chanika umehamishiwa kwa baba yake Chamazi kwa Mkongo.
Spack ambaye amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Aprili 27, 2026 nyumbani kwake Chanika jijini Dar es Salaam alipokuwa anapoishi kwa zaidi ya miaka mitatu sasa aliyejipatia umaarufu mkubwa kupitia kundi la Tip Top Connection, pamoja na nyimbo ya Nipe Ripoti aliyoshikiana na Tundaman.
Malefti amebainisha kwamba usiku wa kuamkia leo alizungumza na msanii huyo kuhusu mpango wao wa 'kushoot' video ya wimbo mpya kabla ya kuagana naye saa saba usiku na kukubaliana kwamba leo wakutane kwa kumuona darekta wa kuandika scripti ya video.
Alisema kwamba asubuhi akiamka ataondoka Chanika kwenda ofisini kwake.
Alisema lakini asubuhi alipogongewa kwa ajili ya kutoa nauli za watoto kwenda shule hakuamka ndipo majirani walipojikusanya kumchukua na kumpeleka hospitali ya Nguvu Kazi iliyopo Chanika ambapo daktari alithibitisha kuwa msanii huyo alikuwa ameshafariki Dunia.

Post a Comment