RAIS DKT. MWINYI: PSSSF IMEKUWA FARAJA KUBWA KWA WASTAAFU ZANZIBAR





Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umekuwa faraja kubwa kwa Wastaafu waliolitumikia taifa hili.

Mhe. Dkt. Mwinyi ameyasema hayo kupitia hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Ikulu, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, katika hafla ya futari ya pamoja iliyoandaliwa na PSSSF kwa ajili ya makundi mbalimbali visiwani Zanzibar (Machi 17, 2026).

“Nachukua fursa hii kuwapongeza PSSSF kwa kuendelea kuwahudumia wanachama wetu, hasa wastaafu, kwani siku hizi ikifika tarehe 25 ya kila mwezi wastaafu hupokea pensheni zao, hongereni sana na muendelee kufanya hivyo, kwa hakika mmekuwa faraja kubwa sana kwa wastaafu wetu,” alisema.

Aidha, Mhe. Dkt. Mwinhyi alisema,katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, binadamu tunakumbushwa kutenda mema.“Nawashukuru kwa kuandaa futari hii ya pamoja lakini pia kwa msaada mliotoa kusaidia makundi mbalimbali hapa Zanzibar.” Alisema.

Akizungumza kwenye futari hiyo ya pamoja Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu, amesema Mwezi huu wa Ramadhani unafundisha umuhimu wa binadamu kuwa na subira, huruma na kusaidiana kwa wale wenye uhitaji katika jamii yetu jambo ambalo PSSSF wamelifanya Zanzibar.






“Kama Waziri ninayesimamia taasisi iliyoandaa futari hii, tutaendelea kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na uwajibikaji ili kuendelea kuwatumikia wananchi kwa haki na usawa.” Alisisitiza Mhe. Sangu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Fortunatus Magambo alisema, katika kipindi hiki ulimwengu mzima, Wakristo na Waislamu wako kwenye Mfungo na wanakumbushwa kufunga, kufanya ibada na kusaidia wenye uhitaji.

Bw. Magambo alisema PSSSF wana Sera ya Huduma kwa Jamii (CSR) ambayo lengo lake ni kusaidia jamii katika maeneo ambayo yameaninishwa kwenye sera na kwa Zanzibar imetoa shilingi milioni 30 ambazo zimekwenda kwenye taasisi tatu ambazo ni Zanzibar National Association of the Blind, Life Lift Foundation na Zanzibar  Albinism Organisation.” Alifafanua Bw. Magambo.


No comments