Kili Marathon Kunoga: Bia ya Kilimanjaro Kuzindua Kampeni Kabambe ya ‘Vyakwetu Vizuri’ Kwa Kishindo
BIA ya Kilimanjaro inatarajia kuzindua rasmi kampeni yake mpya ya ijulikanayo kama ‘Vyakwetu Vizuri’ kwenye wikiendi ya Kilimanjaro Marathon, tukio litakalogeuza mashindano hayo maarufu kuwa jukwaa la kuonesha fahari, utamaduni na umoja wa Watanzania.
Akizungumza kuhusu kampeni hiyo, Mkuu wa Masoko wa Tanzania Breweries Limited, Khensani Mkhombo, alieleza kuwa kampeni hiyo imejengwa juu ya utamaduni wa kila siku wa Mtanzania.
“Vyakwetu Vizuri ni kusherehekea hekima iliyopo kwenye utamaduni wetu. Methali zetu zinatuongoza namna ya kuishi, kupokea wageni na kusonga mbele pamoja. Kilimanjaro Marathon ni nafasi muhimu inayotuunganisha sote, na kampeni hii inaenzi umoja huo” alisema.
Kampeni hiyo itamshirikisha mwanariadha maarufu wa mbio ndefu, Alphonce Simbu, ambaye ameipeperusha vyema bendera ya Tanzania kimataifa.
Kama sehemu ya maadhimisho hayo, Simbu ataongoza utaratibu maalumu wa kuwapa motisha wakimbiaji wa kilomita 42 kupitia wimbo wa hamasa utakaowasaidia kuendelea kupambana hadi mwisho wa mbio.
Akizungumzia uzoefu wake, Simbu alisema: “Nimepitia changamoto nyingi, lakini sikuwahi kukata tamaa. Nimejifunza kuwa ukiwa na nia, unapata njia. Hiyo ndiyo nguvu ya Mtanzania tunasimama pamoja, tunapambana na tunaendelea kuonesha dunia uwezo wetu”.
Kampeni ya ‘Vyakwetu Vizuri’ inalenga kuwakumbusha Watanzania kuwa nguvu yao ya kweli ipo katika umoja, uthubutu na mshikamano wao.
Kwa zaidi ya miaka 20, Bia ya Kilimanjaro imekuwa mdhamini mkuu wa mbio za kilomita 42 za Kilimanjaro Marathon, ikiendeleza dhamira yake ya kudumisha umoja, mafanikio, ukarimu na uzalendo.
Kwa sasa, marathon hii imekuwa zaidi ya mashindano ya riadha na kuwa tukio kubwa la kijamii na kitamaduni linalowaleta pamoja wanariadha, jamii na wageni kutoka ndani na nje ya nchi.
Kwenye kilele cha Kili Marathon mwaka huu, burudani itaongezeka kupitia Kili Dome, tamasha litakalofanyika kuanzia Jumamosi hadi Jumapili.
Washiriki na mashabiki watapata fursa ya kufurahia muziki wa wasanii mbalimbali, vyakula vya asili, pamoja kiburudani kibao.
Wasanii watakaotumbuiza Jumamosi ni Scotts Maphuma
Ali Kiba, Ciza, Joh Makini na Tlhogi_Molefi na Jumapili ni Adekunle Gold, Mbosso, Maphorisa, D Voice na Tlhogi Molefi.
Post a Comment