FURSA ZA AJIRA ZAMWAGWA MIRADI YA MELI ZIWA TANGANYIKA

 



Ufunguzi wa fursa mpya za kiuchumi katika mikoa ya pembezoni mwa Ziwa Tanganyika sasa umepata msukumo mpya baada ya Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) kuruhusu uwekezaji mkubwa wa ujenzi wa meli nne za mizigo katika Bandari ya Karema.

Mradi huu unaotekelezwa na kampuni ya Gold Voyage Logistics kutoka China, umeanza kuleta matumaini kwa wananchi wa Rukwa, Katavi, na Kigoma kwa kuzalisha ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja ambapo kila meli moja inahitaji angalau mabaharia 15.

Akizungumza na waandishi wa habari, South Port mkoani Mwanza alisema pia serikali imewekeza Shilingi bilioni 158.27 katika ujenzi wa meli nyingine mpya ya mizigo Ziwa Tanganyika itakayoweza kubeba tani 3,500 au mabehewa 25 ya reli ya kisasa ya SGR. Meli hii itapunguza muda wa safari kutoka Kigoma hadi Kalemie nchini DRC kuwa saa sita tu.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, akizungumza na waandishi wa habari mjini Mwanza ameeleza kuwa ujenzi wa meli nne za Karema ulioanza Aprili 2025 umefikia asilimia 95 na unatarajiwa kukamilika Julai 2026.

Meli hizo zitakuwa na uwezo wa kubeba kati ya tani 8,000 hadi 10,000 za mizigo kwa wakati mmoja.

Aidha, ukarabati wa meli kongwe ya MV Liemba kwa gharama ya dola za Marekani 13,192,850 sawa na Shilingi bilioni 32.9 unaendelea vyema ukiwa umefikia asilimia 55.

 Uwekezaji mwingine mkubwa ni mikataba yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 625 iliyosainiwa na kampuni ya Dearsan Shipyard ya Uturuki kwa ajili ya ujenzi wa meli mpya mbili na kiwanda cha kujenga meli.

Juhudi hizi ni ushadidi wa namna serikali inavyotumia rasilimali fedha kuboresha maisha ya wananchi na kukuza uchumi wa kikanda kupitia sekta ya uchukuzi.

No comments