SERIKALI YAZINDUA PROGRAMU NA MKAKATI WA KAZI ZA STAHA




Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Clement Sangu amezindua Programu ya Nchi ya Kazi za Staha Awamu ya Tatu ya Mwaka 2025/2026 – 2029/2030 na Mkakati wa kukuza Kazi za Staha Kwa wafanyakazi wa nyumbani.

Aidha, amesema Progamu hii inalenga kuimarisha majadiliano ya kijamii (social dialogue) na mshikamano baina ya Serikali, Waajiri na Wafanyakazi. Pia kuhakikisha wafanyakazi wa nyumbani wapata ulinzi, kutambuliwa na kufikiwa fursa wanazo stahili ili kuongeza kazi za staha.

Uzinduzi huo umefanyika leo Februari 13, 2026 katika ukumbi wa Hoteli ya Best Western, Jijini Dodoma.

Vilevile, Waziri Sangu amesema serikali itaendelea kuwezesha mazingira wezeshi yatakayo rahisisha maendeleo ya programu za kazi za staha.

Kwa upande wake, Kamishna Mkuu wa Kazi,  Suzan Mkangwa amesema Serikali ipo katika mchakato wa kuridhia mkataba wa wafanyakazi wa majumbani, hivyo kukamilika wa Programu ya Nchi ya Kazi za Staha Awamu ya Tatu utasaidia kufanikisha maridhiano ya mkataba huo.







Kadhalika, Kamishna Mkangwa amesema kuwa Serikali imeendelea kuwapatia kipaumbele wafanyakazi wa nyumbani kwa kusimamia maslahi yao na kuwalinda kupitia mifumo ya sheria ikiwemo Sheria ya Mahusiano Kazini ambayo inaainisha viwango vya kazi wote ikiwa ni Pamoja na wafanyakazi wa nyumbani.

Naye, Mkurugenzi Shirika la Kazi Duniani (ILO) Afrika Mashariki, Bi. Caroline Mugala, amesema kazi za staha ni utu hivyo jambo jema nchi wanachama wa ILO kuhakikisha wafanyakazi wanafanya kazi za staha kwa kuwa zinahakikisha haki katika maeneo ya kazi, kinga ya jamii na majadiliano mema katika maeneo ya kazi. 

Ameongeza kuwa utekelezaji wa programu ya kazi za staha itaimarisha Maendeleo ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania.

No comments