RAIS SAMIA AWAAPISHA KABUDI, MAKONDA NA KATAMBI; ATOA MAELEKEZO MAZITO AFCON 2027



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Januari 13, 2026, amewaapisha viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni katika hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

Katika hafla hiyo, Rais Samia amefafanua kuwa uteuzi wa viongozi hao umezingatia uwezo, uzoefu, uadilifu, na rekodi zao nzuri katika utumishi wa umma. Miongoni mwa walioapishwa ni Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi anayekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Ikulu (Kazi Maalum), akitegemewa kutumia uzoefu wake mpana kuimarisha ushauri wa kimkakati wa Serikali.

Maelekezo kwa Mawaziri Wapya Rais ametoa maelekezo mahsusi kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, akimtaka kusimamia kikamilifu maandalizi ya Mashindano ya AFCON 2027 ambayo Tanzania ni mwenyeji. Pia, amemtaka kutumia sekta ya michezo kama chombo cha kutengeneza ajira kwa vijana na kudumisha umoja wa kitaifa.

Kwa upande wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Patrobas Katambi, Rais Samia amemtaka kuimarisha amani, utulivu, na kulinda misingi ya haki na utawala wa sheria ili kuongeza imani ya wananchi kwa Serikali. Viongozi wengine walioapishwa ni pamoja na Katibu Mkuu Dkt. Richard Muyungi (Ofisi ya Makamu wa Rais) na Mabalozi wapya ambao wametakiwa kulinda maslahi ya Tanzania kimataifa

No comments