Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, July 16, 2024

Tanzania mabingwa kikapu U-16 Kanda ya Tano Afrika

 


TIMU ya wasichana chini ya umri wa miaka 16 ya mchezo wa kikapu ya Tanzania imeibuka mabingwa wa mashindano ya Kanda ya Tano Afrika yaliyokuwa yakichezwa katika Kituo cha Michezo cha Filbert Bayi, Kibaha mkoani Pwani.

Mashindano hayo yalianza Juni 12 na kumalizika juzi yakishirikisha timu za wasichana na wavulana kutoka Kenya, Burundi na Tanzania.

Tanzania iliibuka bingwa baada ya kuifunga Kenya kwa pointi 71-69 na kuifunga Burundi kwa pointi 88-17 wakati Kenya waliifunga Burundi kwa pointi 90-15.

Katika michezo ya wavulana Tanzania ilishika nafasi ya pili wakati mabingwa wakiwa Burundi na Kenya mshindi wa tatu.

Burundi waliifunga Tanzania 65-53, Kenya 80-66 na Tanzania iliifunga Kenya 64-62.

Kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja wasichana Tanzania ilitoa 'best pointer' ambaye ni Magdalena Mollel na Namnyak Mollel akiibuka 'best rebounder'.

Kwa upande wa wavulana, Tanzania ilitoa 'best rebounder', Farabi Kanyungilo na mfungaji bora, Venance Kikasa.

No comments:

Post a Comment