Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, July 16, 2024

LIGI KUU TANZANIA BARA KUANZA AGOSTI

LIGI Kuu Tanzania Bara msimu wa 2024/2025 inatarajiwa kuanza Agosti 16 mwaka huu na kumalizika Juni 11 mwakani.

Kwa mujibu wa kalenda ya matukio iliyotolewa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) semina za wasimamizi kuanzia Julai 26 hadi Agosti 2 na mechi za Ngao ya Jamii zitachezwa kuanzia Agosti 8-11 mwaka huu.

NBC Championship League itaanza Septemba 14 mwaka huu na kumalizika Mei 28 mwakani na First League itaanza Novemba 23 mwaka huu itamalizika Mei 24 mwakani.

Msimu uliopita Ligi Kuu ilianza Agosti 15 na itatangazwa kua itafikia tamati Juni 9, mwaka huu lakini ilimalizika Juni 16 mwaka huu ikiwa ni ongezeko la siku saba.

Akizungumza na gazeti hili Ofisa Habari wa TPLB, Karimu Boimanda, alisema baada ya kutoa kalenda ya matukio ya msimu mzima, ratiba ya Ligi Kuu inatarajiwa kutoka wiki hii.

“Ratiba ya Ligi Kuu itatoka ndani ya wiki hii,” alisema Boimanda.

Timu 16 zitakuwa na kazi ya kuwania ubingwa wa Tanzania Bara ambao kwa misimu mitatu mfululizo umekuwa ukitwaliwa na Yanga.

Pia zitawania nafasi nne za juu, ambazo hutoa nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika kwa msimu wa 2025/26.



 


No comments:

Post a Comment