Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, July 24, 2024

KCB EAST AFRICA GOLF TOUR KUFANYIKA LUGALO

 



SHINDANO la wazi la mchezo wa gofu (KCB EAST Africa Golf tour) linatarajiwa kufanyika Agosti 3 mwaka huu katika Viwanja vya Lugalo Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa klabu ya Lugalo, Brigedia Jenerali mstaafu, Michael Luwongo alisema shindano hilo litashirikisha wachezaji 150 kutoka nchi mbalimbali na klabu za hapa nchini.

Luwongo alisema lengo ni kupata timu ya wachezaji wanne watakaokwenda kushiriki mashindano Nairobi, Kenya Desemba 6 mwaka huu.

"Maandalizi ya shindano hili yanaendelea vizuri, mpaka sasa tunaendelea kuboresha miundombinu ya viwanja vyetu ili shindano lifanyike kwa weledi” alisema Luwongo.

Pia aliipongeza Benki ya KCB kwa udhamini wao na kuwataka wale ambao hawajathibitisha ushiriki wao wafanye haraka muda umeisha.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa KCB, Cosmas Kimario alisema benki hiyo inatoa huduma kwa jamii pamoja na michezo mbalimbali ikiwemo riadha, mpira wa miguu na ngumi.

"Tuna uhakika hii timu itakayokwenda Kenya itafanya vizuri na kurudi na ushindi nyumbani, ili fainali ijayo ifanyika hapa nchini, alisema Kimario.

Alisema wameamua kuwekeza katika michezo kwa lengo la kukuza vipaji vya vijana wadogo wanaochipukia.

Naye nahodha wa klabu ya Lugalo, Meja Japhet Masai alisema shindano hilo litachezwa kwa mfumo wa kuhesabu mashimo kwa pointi na atakayepata pointi nyingi atapata nafasi ya kwenda Kenya.

No comments:

Post a Comment