Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, July 24, 2024

TIMU YA TAIFA YA MICHEZO YA OLIMPIKI UFARANSA 2024 YAWASILI PARIS


Kundi la kwanza la wachezaji wa Tanzania watakaoiwakilisha nchi katika  Michezo ya Olimpiki limewasili salama asubuhi ya leo Julai 24, 2024 jijini Paris nchini Ufaransa.

Kundi hilo la kwanza lina waogeleaji wawili, Sofia Anisa Latiff na Collins Phillip  Saiboko na mwalimu wao Alexander Harrison Mwaipasi pamoja na Daktari wa timu, Dkt Eliasa Abdallah Mkongo. 

Waogeleaji wataanza kuchuana Agosti 30 mwaka huu, ambapo Collins Phillip Saiboko atashindana katika michuano ya mita 100 Freestyle kwa wanaume huku, Sofia Anisa Latiff atashindana Agosti 3,  katika mita 50 freestyle kwa wanawake.

Mwingine aliyewasili leo Paris ni mwalimu wa mchezo wa Judo, Innocent John Mallya, ambaye mchezaji wake, Andrew Thomas Mlugu (Kg 73), tayari yupo Paris kwa mwaka mmoja katika kambi maalumu ya mazoezi ya CRJ Centre iliyoandaliwa na Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa (IOC) na ataanza kuingia dimbani Agosti 2 mwaka huu.

Wanamichezo wanne, ambao wote ni wakimbiaji wa Marathon, bado wako kambini Jijini  Arusha wakiendelea kujifua na wanatarajiwa kuwasili Paris Augosti 7 na Marathon itakuwa Agosti 11, 2024.

Wanariadha hao wa marathon ni wanaume Alphonce Felix Simbu na Gabriel Geay, na wanawake ni  Jackline Juma Sakilu na Magdalena Crispin Shauri.

No comments:

Post a Comment