Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, July 24, 2024

SIMBA YAMCHUKULIA KIBU MTORO KAZINI

 

UONGOZI wa Simba umesema kitendo cha mshambuliaji Denis Kibu kutokuwepo kambini hakiathiri mipango yao ila watamchukulia hatua za kinidhamu kwa kosa hilo.

Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally Morogoro leo walipokwenda kuzindua jezi mpya za msimu ujao.

Kibu aliongezewa mkataba wa miaka miwili utakaomalizika Juni 2026 na kulipwa stahiki zake za kimkataba jambo ambalo hata meneja wake Carlos Mastermind amekiri mchezaji huyo haidai Simba.

Ahmed alisema kutokuwepo kwa Kibu hakuathiri programu za Kocha Mkuu Fadlu Davis kwa sababu wamefanya usajili kulingana na mahitaji ya timu.

“Kibu hadi sasa hajaungana na timu nchini Misri. Tulimuongeza mkataba wa miaka miwili na amesaini kuitumikia Simba, tumemlipa fedha zote na mahitaji yote aliyohitaji. Amelipwa kama kondakta, fedha alikabidhiwa mkononi na kuondoka, hatuna deni na mchezaji bali Simba inamdai utumishi wake,” alisema Ahmed.

Pia alisema baada ya kumaliza ligi alienda Marekani lakini walimpa taarifa ya kambi, kupima afya na safari ya Misri, baadaye alisema hati ya kusafiria imejaa.

“Kweli alirudi na kufuatilia hati yake lakini hakutokea ofisini kwa ajili ya safari, alipotafutwa apeleke hati yake akasema ameenda Kigoma, baada ya hapo zikaanza danadana za hapa na pale, tutaendelea kumtafuta lakini jana tulisikia ameenda nje ya nchi,” alisema Ahmed.

Tetesi zinasema Kibu amevutiwa na Yanga na anaweza kutambulishwa Siku ya Wananchi itakayofanyika Agosti 4 Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Endapo atasajiliwa Yanga haitakuwa ajabu kwani meneja wake Carlos pamoja na kukiri Simba kumlipa stahili zote alidai Yanga ndio waliotoa dau kubwa.

Hata hivyo Carlos anasema mchezaji huyo amepata mwaliko wa moja ya klabu nchini Norway.

“Ni kweli Kibu hajajiunga na timu Misri kwa sasa yupo Ulaya, ninachojua hawadai Simba wamemalizana na suala la kwanini hajajiunga na wenzake nchini Misri, Simba wana uwezo wa kujibu hilo,” alisema Carlos.

No comments:

Post a Comment