KAZI ya
kukarabati Uwanja wa Taifa inatarajiwa kumalizika Novemba 21 na unakabidhiwa
serikalini Novemba 24.
Hayo
yalisemwa na Mkuu wa Operesheni SportPesa Luca Neghesti leo wakati kamati ya
maandalizi ya fainali za Afrika (afcon U-17) ilipokagua uwanja huo ikiongozwa
na Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe.
“Kazi ya
kukarabati sehemu ya kuchezea imekamilika na nyasi zilizooteshwa zimeota vizuri
na zimeshika hivyo upo tayari kutumika,” alisema Luca.
Akizungumza
Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe
aliishukuru SportPesa ambao ndio wanakarabati uwanja huo.
“Nashukuru
kuona uwanja nyasi zimeota vizuri na unapendeza na kikubwa nashukuru kwa vijana
wetu sita ambao wamefundishwa namna ya kutunza viwanja,” alisema Dk. Mwakyembe.
Pia
Mwakyembe alisema vijana sita waliopata mafunzo hayo ni mmoja tu ndio aliyeajiriwa
serikali na kuwasihi kuwa wavumilivu wakati wakifanya mchakato wa ajira zao.
Aidha
alitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuandaa mchezo wa ligi ambao
utachezwa Novemba 24 kwa ajili ya kukabidhiwa uwanja, jambo ambalo Kaimu Katibu
Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao alisema wataangalia namna ya kupata mchezo kwani
inawezekana ratiba ikawa imesimama kupisha Chalenji.
“Tutaangalia
kwani leo na kesho tutakuwa na kikao na boodi ya ligi kwa ajili ya kufanya
mabadiliko ya ligi kwani timu za Taifa ya bara na ile ya Zanzibar zitakuwa
kwenye mashindano ya Chalenji inayotarajiwa Novemba 25,” alisema Kidao.
No comments:
Post a Comment