TIMU ya Taifa ya soka ya
Tanzania ‘Taifa Stars’, imetoka sare ya kufungana bao 1-1 na Benin katika
mchezo wa kirafiki wa Kimataifa utakaochezwa katika dimba la Stade de I’Amitie
mjini Cotonou.
Benin
ambao walikuwa wamepania kulipiza kipigo cha mabao 4-1 walichopata mwaka 2014
kwenye Uwanja wa Taifa walijikuta wakiambulia sare hiyo ambayo ilitokana na
mwamuzi kutokuwa makini.
Bao
la Benin lilifungwa dakika ya 32 na nahodha
mkongwe Stephane Sessegnon kwa penalti baada ya
mwamuzi Ligali Praphiou kuashiria pigo hilo kwa madai kuwa Gadiel wa Taifa Stars ndie
ameshika wakati aliyeshika alikuwa mchezaji wao Khaled Adenon.
Maamuzi hayo
yalionekana kuwachanga wachezaji wa Taifa Stars lakini walijipanga na kutulia
na kucheza mpira na dakika ya 39 Simon Msuva alipiga shuti ambalo lilienda
langoni lakini kipa alilipangua vizuri.
Kipindi cha pili
Taifa Stars walicheza pasi fupi ambazo zilisaidia kupata bao dakika ya 50
lililofungwa na Elias Maguli kwa kisigino akiunganisha pasi ya Shiza Kichuya.
Kama vile kocha
wa Taifa Stars alihitaji kufunga mabao zaidi alimtoa kiungo Rafael Daudi na
kuingiza mshambuliaji Mbaraka Yusuf, Shiza Kichuya nafasi yake ikachukuliwa na
Ibrahim Ajib, Hamis Abdallah akaingia Jonas Mkude baadae akaumia Mudathir
akaingia Nurdin Chona.
Kwa matokeo hayo huenda
Tanzania ikapanda katika viwango vya FIFA ambayo hutolewa kila mwezi kwani Benin
inashika nafasi ya 79 na Tanzania inashika nafasi ya 136 katika viwango vya
Oktoba.
Tanzania; Aishi Manula, Himid Mao, Gardiel Michael, Abdi Banda, Kelvin Yondan, Hamisi Abdallah/Jonas Mkude dk 75, Simon Msuva/Boniphace Maganga dk 85, Mudathir Yahya/Nurdin Chona dk 92, Elias Maguli, Raphael Daudi/Mbaraka Yusuph dk 54 na Shizza Kichuya/Ibrahim Ajib dk 65
Kikosi cha
Benin kilikuwa; Fabien Farnole, Rodrigue Fassinou, Khaled Adenon, Cedric
Hountonji, David Kiki, Djiman Koukou, Olivier Verdon, Jodel Dossou, Stephane
Sessegnon, David Djigla Dossou na Steve Mounie.
No comments:
Post a Comment