SERIKALI
imeunda kamati ya maandalizi ya fainali za soka za Vijana za Afrika (AFCON
U-17) zilinazotarajiwa kufanyika nchini 2019.
Akizungumza leo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe alisema kamati hiyo
ina watu 25 na imefanya kikao chake cha kwanza leo.
“Tanzania
kama nchi tuna mtihani mgumu na mtihani huu ni lazima kufaulu hivyo serikali
imeunda kamati ya watu 25 ambayo ndani yake zitapatikana kamati nyingine ndogo
ndogo,” alisema Dk. Mwakyembe.
Pia alisema
2019 ipo karibuni ndio maana kikao cha kwanza kilichokaa jana wajumbe walichagua
mwenyekiti wa kamati na makamu wake pamoja na mtendaji wa kamati.
“Kamati
hiyo, mimi ndio nimechaguliwa kuwa mwenyekiti na Leodgar Tenga amechaguliwa
kuwa makamu na mtendaji wa kamati amechaguliwa Henry Tandau na wajumbe wote
walioteuliwa wamekubali,” alisema Dk. Mwakyembe.
Wajumbe ni
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Makamu wa Rais wa TFF, Michael
Wambura, Mkuu wa kitivo cha sheria Chuo Kikuu Huria, Dk. Damas Ndumbaro, Dk.
Francis Michael kutoka kitivo cha sheria
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Waziri wa
Maliasili na Utalii Dk Hamis Kigwangala, Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Allan
Kijazi, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James,Kamishna Jenerali wa
Idara ya Uhamiaji Dk. Anna Makakala, Mkurugenzi Mtendaji wa Ngorongoro kreta Dk.
Freddy Manongi.
Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya Mohamed Enterprises Ltd, Mohammed Dewji, Mkurugenzi Mtendaji
Said Salim Bakhresa &Co Ltd, Abubakar Bakhresa, Mkurugenzi wa Maendeleo ya
Michezo wa Wizara wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Yusuph Singo.
Mkurugenzi
Mkuu wa PPF Wiliam Erio, Mkurugenzi Mkuu Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,Dk.
Lawrance Maseru, Mtendaji Mtendaji wa ATCL, Eng. Ladislaus Matindi, Mtendaji wa
Bodi ya Utalii Tanzania, Devotha Mdachi na
Ofisa Masoko Mkuu wa SportPesa, Kelvin Twisa
Mkurungezi
wa Manispaa ya Temeke Nassib Mmbagga, Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya
TFF, Ahmed Mgoyi, Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Vijana ya TFF, Khalid
Abdallah, Angetile Osiah kutoka Mwananchi Communications, Lameck Nyambaya
mjumbe wa kamati ya Utendaji TFF.
Tanzania ni
mara ya kwanza kuandaa fainali za mashindano ya soka ya Afrika hivyo ni nafasi
pekee ambayo inapaswa kutumika vema kwani itaitangaza nchi katika kimataifa
katika uchumi, raslimali, na hata kutangaza wachezaji wetu
No comments:
Post a Comment