FAIDHA KASSIM AIWEKA TANZANIA RAMANI YA DUNIA MISS INTERCONTINENTAL 2025

 



Mwakilishi wa Tanzania, Faidha Kassim, ameandika historia baada ya kuibuka mshindi wa tatu (2nd Runner-up) katika fainali za mashindano ya urembo ya Miss Intercontinental 2025 zilizofanyika nchini Misri.

Katika kilele cha mashindano hayo yaliyoshirikisha warembo kutoka mataifa mbalimbali, Faidha aling’ara si tu kwa urembo na kipaji, bali pia kwa kupata uungwaji mkono mkubwa. Alifanikiwa kutwaa tuzo ya Mshindi wa Kura za Mtandaoni (People’s Choice), ikiwa ni ishara ya upendo na sapoti kubwa aliyopata kutoka kwa Watanzania na mashabiki wa urembo duniani kote.

Washindi na Mataji Mengine

Taji kuu la Miss Intercontinental 2025 lilinyakuliwa na Varvara Yakovenko wa Urusi. Mbali na taji hilo, Yakovenko pia aliondoka na tuzo za Malkia wa Ulaya na Miss Photogenic.

Msimamo wa washindi saba bora ulikuwa kama ifuatavyo:

  • Mshindi wa Pili: Lorena Suarez Lara (Cuba) – Pia alitawazwa kuwa Malkia wa Amerika Kaskazini.

  • Mshindi wa Tatu: Faidha Kassim (Tanzania).

  • Mshindi wa Nne: Vanessa Nattacha Wenk (Thailand) – Malkia wa Asia na Oceania.

  • Mshindi wa Tano: Christina Labareño Vanhefflin (Ufilipino) – Aliyetwaa pia tuzo ya Power of Beauty.

  • Mshindi wa Sita: Christiane Guerrero Marques das Neves (Ecuador) – Aliyeshinda tuzo ya Miss Congeniality na Malkia wa Amerika Kusini.

  • Mshindi wa Saba: Brilliant Maroko (Kenya) – Aliyetwaa taji la Malkia wa Afrika na tuzo ya Best in Swimsuit.

Mafanikio kwa Tanzania

Ushindi huu wa Faidha Kassim unatajwa kuwa moja ya mafanikio makubwa kwa tasnia ya urembo nchini Tanzania kwa mwaka 2025. Kupenya kwake hadi hatua ya tano bora na hatimaye kushika nafasi ya tatu, kunathibitisha uwezo wa warembo wa Kitanzania katika majukwaa ya kimataifa.

Ushindi wake wa kura za mtandaoni unadhihirisha nguvu ya umoja wa Watanzania katika kuwasapoti wawakilishi wao wanapopeperusha bendera ya taifa nje ya nchi.

No comments