Akizungumza leo Ofisa Mtendaji wa bodi ya ligi , Boniface Wambura alisema Simba imetozwa
faini y ash. 300,000 kwa kuwasilisha orodha ya wachezaji katika mchezo dhidi ya
Mbeya City vilevile imepewa onyo kali kutokana na kocha msaidizi Djuma Masoud
kuanza kufundisha bila ya vibali vya kuishi na kufanya kazi nchini.
”Klabu ya Simba imepewa onyo kutokana na kocha wake msaidizi Masoud
Djuma kuanza kufundisha bila kuwa na vibali vya kuishi na kufanya kazi nchini
chini ya kanuni ya 40(13) ya Ligi Kuu kuhusu udhibiti wa makocha hivyo Simba
inatakiwa kabla ya Novemba 10 iwe imewasilisha Bodi ya Ligi nakala ya vibali
hivyo kwani kwa kuwa mahitaji ya nyaraka hizo ni kwa mujibu wa kanuni za ligi,
lakini pia sheria za nchi,” alisema Wambura.
Pia Wambura alisema Yanga imetozwa faini ya sh 500,000
kutokana na mashabiki wake kurusha chupa zinazosadikiwa kuwa na mikojo wakati
wa mchezo dhidi ya Simba uliochezwa Uwanja wa Uhuru na kumalizika kwa sare ya
1-1 na adhabu hiyo imezingatia kanuni ya 42(1) ya udhibiti wa klabu.
Aidha Njombe Mji imepigwa faini ya sh. 500,000 (kutokana
na kuonesha vitendo vinavyoashiria imani za ushirikina katika mchezo dhidi ya
Simba wakati ikiwasili uwanjani.
Vilevile Stand United imetozwa faini ya sh. 300,000
kutokana na golikipa wao kuvaa jezi yenye namba tofauti na ile iliyosajiliwa, kitendo
ambacho ni ukiukaji wa kanuni ya 60(11) ya Ligi Kuu kuhusu usajili na adhabu
imezingatia kanuni ya 60(12)
Naye mwamuzi Shakaile Ole Yangalai na
kamishna wake David Lugenge wamefungiwa miezi mitatu kwa kutoripoti na kuchukua
hatua dhidi ya kitendo cha Kipa Owen Chaima wa Mbeya City kumpiga kofi
mshambuliaji wa Azam FC, Yahaya Mohamed.
No comments:
Post a Comment