TIMU za Mgambo JKT imepigwa faini ya sh. 500,000 kutokana na
washabiki wake kuingia uwanjani baada ya filimbi ya mwisho ya mchezo kupulizwa
na Kiluvya United imepigwa faini ya sh. 100,000 kwa kutohudhuria kikao cha
maandalizi ya mechi.
Friends
Rangers imepigwa faini ya sh. 500,000 kutokana na washabiki wake kusababisha
mchezo kusimama kwa dakika tano baada ya kumpiga jiwe mwamuzi msaidizi na JKT
Mlale imepigwa faini ya sh. 100,000 kutokana na kuhudhuria kikao cha maandalizi
ya mechi ikiwa na maofisa pungufu
Mawenzi
Market imepigwa faini ya sh. 500,000 kutokana na washabiki wake kusababisha
mchezo kusimama kwa dakika nne baada ya kumpiga jiwe mwamuzi msaidizi.
Transit Camp
na Biashara United Mara kila moja imepigwa faini ya sh. 500,000 kutokana na
vitendo vinavyoashiria imani za ushirikina katika mechi hiyo wakati zikiingia
uwanjani vilevile Transit Camp pia imepigwa faini ya sh. 500,000 kutokana na
washabiki wake kuingia uwanjani baada ya mchezo kupmalizika kwa lengo la kutaka
kumpiga mwamuzi.
Naye
mchezaji wa KMC Stephano Mwasika amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh.
300,000 kwa kumpiga kiwiko kwa makusudi mchezaji wa Mbeya Kwanza na Athuman Idd
Chuji wa Coastal Union na Shabani Stambuli wa Polisi Tanzania wamesimamishwa
mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 300,000
Na katika
daraja la pili Pepsi imepigwa faini ya sh. 100,000 (laki moja) kwa kuchelewa
kwenye kikao cha maandalizi na pia kuchelewa kufika uwanjani na Kilimanjaro
Heroes, African Sports, Mkamba Rangers, Milambo na Mashujaa zimepewa onyo
kutokana na makosa mbalimbali.
No comments:
Post a Comment