WAKATI
Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara, ikitarajiwa kuanza Novemba 26, 2017 katika
vituo viwili vya Dar es Salaam na Arusha, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
limesema huu ni wakati wa pingamizi baada ya usajili wa msimu huu kwa timu zote
12, kukamilika juzi.
Akuzungumza
na wandishi wa habari leo, Ofisa habari wa TFF Alfred Lucas alisema mwisho wa
kupokea pingamizi ni Novemba 17.
“Kipindi
cha usajili kilikuwa Oktoba 25 hadi Novemba 12 na kuanzia jana hadi Novemba
17, ni kipindi cha pingamizi hivyo viongozi wa timu wanatakiwa kuwasilisha pingamizi
kama yapo,” alisema Lucas
Pia
alisema Novemba 18, Kamati ya Sheria itakaa kutoa leseni za wachezaji na Novemba
24, kutakuwa na semina ya viongozi wa klabu, Waamuzi na Makamishna Dar es
Salaam.
Wakati
huo huo Lucas alisema Vikosi vya timu za soka za Taifa ya Kilimanjaro Heroes na
Serengeti boys vitatangwa wiki ijayo kwa ajili ya kuingia kambini kujiandaa na
mashindano ya Baraza la michezo kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Lucas
alisema Kilimanjaro Heroes inajiandaa na ambayo inatarajiwa kufanyika Kenya
kuanzia Novemba 25 hadi Desemba 9 na Serengeti inajiandaa na mashindano kama
hayo kwa timu za U-17 ambayo yanatarajiwa kufanyika Rwanda kuanzia Desemba
12-22.
Aidha
Taifa Stars ilirejea usiku wa kuamkia jana toka Benin ambapo walikwenda kucheza
mchezo wa kirafiki wa kimataifa na kutoka sare na wachezaji wote wameshaondoka
kurudi katika timu zao.
No comments:
Post a Comment