Kampuni ya Bia
ya Serengeti (SBL) ambao ni wadhamini wakuu wa timu ya taifa, Taifa Stars,
wameelezea kuvutiwa na kiwango cha soka kilichoonyeshwa na timu hiyo katika
mchezo wake dhidi ya Benin.
Juzi (Jumapili)
Taifa Stars ilitoka droo ya goli moja kwa moja katika mchezo wa kirafiki dhidi
ya timu ya taifa ya Benin uliochezwa
katika jiji la Porto-Novo nchini Benin
Akiongea jana,
Mkurugenzi wa Masoko wa SBL Ceaser Mloka
alisema,kiwango cha Taifa Stars kimekuwa kikiridhisha na kutia moyo tangu
kampuni hiyo iingia udhamini nayo.
Alisema, ni
japo la kutia moyo kwamba tangu SBL itoe udhamini, Taifa Stars haijapoteza
mechi yoyote, iwe ni nyumbani au
ugenini.
“Tukirejea
kwenye mechi ya Jumapili dhidi ya Benin, kama Benin wasingepata penati ni wazi
kuwa Taifa Stars wangeibuka washindi,” alisema
Mkurugenzi huyo
alifafanua kuwa, Taifa Stars walicheza vizuri katika mechi hiyo pamoja na
kwamba Benin wako mbele yao katika nafasi za Shikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA). Kwa mujibu wa viwango vya FIFA Benin
inashikilia nafasi ya 86 huku Tanzania ikishikilia nafasi ya 136.
Ceaser alisema
kukosekana kwa wachezaji muhimu wawili wa Taifa Stars Mbwana Sammata na Thomasi
Ulimwengu kutokana na kuwa majeruhi pia kumeathiri matokeo huku akisisitiza
kuwa timu inaendelea kuboreka
Mwezi Mei mwaka huu, SBL iliingia mkataba wa mitatu na Shirikisho la
Mipira wa Miguu Tanzania (TFF) wa thamani ya shilingi bilioni
2.1 ambao uliifanya kuwa mdhamini mkuu wa timu ya taifa
-Taifa Stars.
Udhamini huo ni wa mara ya pili kwa SBL kuiunga mkono timu ya taifa
baada ya kampuni hiyo kufanya hivyo kwa kipindi cha miaka mitatu ilipoidhamini
timu hiyo kati ya mwaka 2008 hadi 2011.
Uamuzi wa kampuni hiyo wa kuidhamini
timu ya taifa unatokana na sera ya SBL ya kusaidia kuleta maendeleo katika
sekta mbalimbali za kijamii ikiwemo michezo.
No comments:
Post a Comment