SHIRIKISHO
la Soka Tanzania (TFF) limemtangaza Ammy Ninje kuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa
ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ ambayo inajiandaa na mashindano ya Chalenji
ambayo yanatarajiwa kuanza Desemba 3-17 Nairobi.
Akizungumza leo wakati akimtambulisha, Ofisa habari wa TFF, Alfred Lucas alisema kocha huyo kesho anatarajiwa kutangaza kikosi kitakachoshiriki michuano ya kombe la Chalenji kwa
nchi za Afrika Mashariki na Kati.
“Ninje siyo
mgeni kwenu mmemuona kwenye benchi la Taifa Stars takribani michezo miwili,
hivyo ndio atakayekiongoza kikosi cha Kilimanjaro Stars kwenye mashindano ya
Chalenji yatakayofanyika Nairobi,” alisema Lucas.
Akizungumza
baada ya kutambulishwa, Ninje alisema kazi ya kocha siyo kuongea bali ni
kuonesha kwa vitendo kile kilichomo ndani yake, nakuomba ushirikiano kwa wadau
ili timu atakayotangaza leo ifanye vizuri na hatimaye itwae kombe la Chalenji.
“Nashukuru
kwa TFF kuniamini na kunikabidhi timu ya Kilimanjaro Stars ambayo imepangwa
kundi A pamoja na timu za Libya, Rwanda na
wenyeji Kenya,” alisema Ninje ambaye ni kocha mwenye leseni A ya UEFA.
Kabla ya
kuwa kocha Ninje aliwahi kucheza soka la kulipwa katika nchi za Afrika Kusini
1996 timu za Hellenic FC na baadae Wynberg St Jones kabla ya kujiunga na Sparta Rotterdam (Mutual) FC ya China pia alicheza
katika nchi za Denmark,
USA, Scotland na England.
Kwa sasa Ninje
mwenye taaluma ya Uhasibu anafundisha timu ya Vijana ya klabu za Hull City na Notts County na baadhi ya wachezaji
maarufu waliwahi kupitia katika mikono yake ni Josh Tymon, Josh
Clackstone, Harvey Rodgers, Dan James, Max Clarke, Colby Bishop, Lartey
Sarpong, Luther Wilder, Jack McMillian, Montel Gibson, Alex Penny, Jordan
Richards, Harry Caldwell na Rory Watson.
No comments:
Post a Comment