KOCHA Mkuu
wa timu ya Taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’, Ammy Ninje ametangaza
kikosi cha wachezaji 20 ambao wanatarajia kuingia kambini Novemba 26 kwa ajili
ya kujiandaa na mashindano ya Chalenji yatakayofanyika nchini Kenya.
Akizungumza leo Ninje ambaye aliteuliwa jana kushika mikoba hiyo alisema atakuwa
anafundisha darasani na baadae kwa vitendo uwanjani ili kuwapa wepesi wachezaji
kuelewa.
“Nitakuwa
naangalia katika maadili ya timu, nitaongea na wachezaji na kuwaeleza kuwa timu
ya Taifa ni kuwa balozi ili kuwabadilisha mtazamo,” alisema Ninje.
“Kikosi hiki
nimeshirikiana na Kocha wa Taifa Stars Salum Mayanga kwasababu mimi nina muda
wa miezi mitatu tangu niwe kwenye benchi la Taifa Stars,” aliongeza Ninje.
Pia Ninje
alisema anataka kuwasaidia wachezaji kisaikolojia ili waende mbele kimpira
kwasababu Argentina na Brazil wana maisha magumu kama Tanzania lakini wapo
wanacheza soka Ulaya.
Aidha
alisema anapenda wachezaji ambao wanapenda kujifunza na wapo tayari kujifunza
Kikosi hicho
kinaundwa na makipa Aishi Manula (Simba), na Peter Manyika (Singida United).
Walinzi ni
Gadiel Michael na Kelvin Yondani (Yanga), Bonipha Maganga (Mbao FC), Kennedy
Juma (Singida United), Mohammed Hussein na Erasto Nyoni (Simba)
Viungo wa
kati ni Himid Mao (Azam FC) ambaye atakuwa nahodha, Hamis Abdallah (Sony
Sugar/Kenya), Mzamiru Yassin (Simba) na Raphael Daud (Yanga).
Viungo wa
pembeni ni Shizza Kichuya na Jonas Mkude (Simba), Abdul Hilal (Tusker/Kenya),
Ibrahim Ajib (Yanga) na washambuliaji ni Elias Maguli (mchezaji huru), Mbaraka
Yussuph (Azam FC), Danny Lyanga (Fanja Oman) na Yohana Mkomola (mchezaji huru).
Benchi la ufundi
linaundwa yeye NinjeKocha Mkuu, Fulgence Novatus (Kocha Msaidizi), Patrick
Mwangata (Kocha wa makipa), Danny Msangi (Meneja), madaktari ni Richard Yomba
na Gilbert Kigadye na Ally Ruvu (Mtunza Vifaa).
mashindano
ya Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) yanatarajiwa kuanza
Desemba 3-17 , Nairobi Kenya na Kilimanjaro Stars imepangwa kundi A pamoja na
timu za Libya, Rwanda na wenyeji Kenya
No comments:
Post a Comment