SHIRIKISHO
la Soka Tanzania (TFF) limesema litawachukulia hatua za kisheria watu ambao
wataeneza na kusambaza habari ambazo hazina ukweli kuhusu shirikisho hilo.
Hayo
yamesemwa leo na Kaimu Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao wakati akitoa ufafanuzi
wa ujumbe/habari iliosambaa kwenye
mitandao ya kijamii kuongeza posho kwa wajumbe wa kamati ya utendaji pamoja na
kuanzisha malipo ya mishahara kwa Rais na Makamu wake.
Kidao
alisema viwango vya posho za vikao vya Kamati ya Utendaji havijawahi kujadiliwa
wala kubadilishwa (kuongezwa) tangu uongozi mpya uingie madarakani bali kamati
ilipitisha posho y ash. Milioni 1.5 kwa wajumbe kwa miezi mitatu ili iwasaidie
kutekeleza majukumu yao.
“Wajumbe wa
kamati ya utendaji wanawezeshwa kutekeleza majukumu yao kwenye kanda zao kwa
kulipwa sh. Milioni 1.5 ambayo ni sawa na laki tano kila mwezi na hii posho
anapewa baada ya kuwasilisha taarifa ya kazi ambazo amezifanyaka katika kipindi
cha miezi mitatu kwenye kanda yake,” alisema Kidao.
Kidao
alisema kuhusu mshahara wa Rais wa TFF na Makamu wake hilo halikufikiwa mwafaka
kwani halikufuata taratibu japo wajumbe wa kamati ya utendaji walishauri ofisi
ya Rais ihudumiwe na TFF kama ilivyo kwa ofisi za marais wa FIFA na CAF.
“Rais wa TFF
Wallace Karia alikataa kwa kusema, anaamini sio wakati mwafaka wa yeye kuchukua
posho hadi taasisi itakapokaa vizuri na taratibu zote kufuatwa na pia yeye ni mtumishi wa serikali hawezi
kupokea mshahara miwili kwa wakati mmoja,” alisema Kidao.
Kidao ambaye
katika mkutano huo alikuwa ameambatana na wakurugenzi wapya akiwemo Mkurugenzi
wa Wanachama na Sheria, Edward Mwakingwe alimwagiza kuanza kufanya taratibu za
kuwafikisha mahakama watu wote waliosambaza taarifa hiyo kwani ina lengo la
kuichafua taasisi hiyo.
“Nakuagiza
mwanasheria wa TFF, kufungua mashtaka kwa wale waliosambaza ujumbe kwenye
mitandao ya kijamii wenye lengo la kuichafua taasisi hiyo kwani sheria ya
mitandao inakataza kusambaza habari ambazo zinalengo la kuchafua na kuharibu
twasira ya taasisi,” alisema Kidao.
Pia Kidao
alisema ofisi yake ipo wazi muda wote endapo kuna habari wanataka kupata
ufafanuzi wasisite kumpigia na endapo wataona simu haipokelewi watu ujumbe
mfupi maana inawezekana akawa yupo kwenye kikao.
Katika kikao
hicho aliwatambulisha wakurugenzi wapya ambao ajira zao zilipitishwa na kamati
ya utendaji ambao ni Mkurugenzi wa Wanachama na Sheria, Edward Mwakingwe,
Mkurugenzi wa Masoko Aaron Nyanda, Mkurugenzi wa Mashindano Efrem August na
Mkaguzi wa ndani John Benjamin
No comments:
Post a Comment