JUSTIN BIEBER AZUA TAHARUKI GRAMMY 2026: APANDA JUKWAANI NA BOKSA
Mwanamuziki nguli Justin Bieber ameacha gumzo la aina yake katika usiku wa tuzo za Grammy 2026 baada ya kupanda jukwaani akiwa amevua shati na kubaki na boksa ya rangi ya fedha pamoja na soksi pekee.
Katika onyesho hilo lililofanyika Jumapili ya Februari 1 kwenye uwanja wa Crypto.com Arena jijini Los Angeles, Bieber mwenye umri wa miaka 31 alionyesha mchoro wa chale kifuani mwake huku akitumbuiza wimbo wake ulioshika chati wa "Yukon" akitumia gitaa la rangi ya zambarau.
Wakati akimwaga sauti yake jukwaani, mke wake mrembo, Hailey Bieber, alionekana akitabasamu kwa fahari na kumpigia makofi mumewe wakati kamera zilipomulika upande wake.
Kabla ya kupanda jukwaani kwa staili hiyo ya aina yake, wanandoa hao walivutia macho ya wengi kwenye zulia jekundu ambapo Justin alivaa suti kubwa ya Balenciaga na mkufu wa thamani wa karati 100, huku Hailey aking'ara kwa vazi jeusi la Alaïa lililoonyesha umbo lake vyema.
Usiku huo ulikuwa wa furaha kubwa kwa familia hiyo kwani albamu ya Justin iitwayo "Swag" imepata uteuzi wa Albamu Bora ya Mwaka, huku nyimbo zake kama "Daisies" na "Yukon" zikiwania tuzo katika vipengele vya Pop na R&B.
Wimbo wa "Yukon" una maana ya pekee kwake kwani mke wake na mtoto wao, Jack Blues, walionekana kwenye video ya wimbo huo iliyoongozwa na Cole Bennett.
Kupitia albamu hii ya kwanza tangu ile ya "Justice" ya mwaka 2021, Justin anaonekana kuonyesha ukomavu wa penzi lake kwa Hailey, akisisitiza katika nyimbo zake kuwa amebadilika na hana mpango wa kuondoka kwenye himaya ya malkia huyo licha ya changamoto za kimaisha wanazopitia hadharan


Post a Comment