TIMU ya
Vijana Rangers imefuzu robo fainali ya mashindano ya Ndondo baada ya kuifunga
Temeke Squad bao 1-0 kwenye mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Kinesi Urafiki,
Dar es Salaam.
Katika
mchezo huo ambao ulijaa wachezaji chipukizi tofauti na timu zingine ambazo
zimesheheni wachezaji mastaa wa Ligi Kuu, Vijana walipata bao dakika ya 28
lililofungwa na Yahaya Mbegu kwa mpira wa adhabu kubwa nje ya eneo la penalti.
Baada ya bao
hilo kila timu ilijaribu kushambulia lango la mpinzani lakini umahiri wa makipa
ulifanya dakika 90 zikamilike ubao ukisomeka Vijana 1 na Temeke 0.
Katika
mchezo huo mshambuliaji wa Vijana Rangers, Yahaya Mbegu alichaguliwa kuwa
mchezaji bora wa mchezo huo na kupewa sh. 50,000, Vijana Rangers nayo ikaondoka n ash. 150,000
na Temeke Squad 100,000 kutoka kwa kampuni ya mcheza Tanzania.
Kwa matokeo
hayo Vijana imeungana na Goms United, Mlalakuwa Rangers, Mpakani Kombaini
kufuzu nusu fainali na leo kutakuwa na mchezo kati ya Kibada One na Kigogo.
No comments:
Post a Comment