MENEJA
wa Manchester United Jose Mourinho amesisitiza Kipa David De Gea
atabaki kuwa Mchezaji wao kwa Msimu ujao huku pia akisema nia yake ni
kupata Mchezaji Mmoja Mpya au Wawili lakini Fowadi wa Real Madrid Gareth
Bale si mmoja wao.
DAVID DE GEA
Jose Mourinho amesisitiza David De Gea atabakia Manchester United kwa Msimu ujao kwani Kipa huyo hana nia kujiunga na Real Madrid kama inavyozushwa.
Kwenye Duru nyingi za Soka ilivumishwa kuwa Real Madrid itatoa Ofa kumnunua De Gea baada ya kumkosa Dakika za mwisho za Siku ya Mwisho ya Dirisha la Uhamisho Mwaka 2015.
Mourinho ameeleza: "Nawahakikishieni De Gea hahami Msimu huu!"
Vile vile Mourinho ametoboa De Gea amekiri uwepo wa Kipa wa Akiba Sergio Romero ambae pia hudakia Timu ya Taifa ya Argentina kumemfanya awe bora zaidi.
Mourinho ameeleza kwa jinsi Romero alivyodaka Msimu uliopita, hasa kwenye UEFA EUROPA LIGI, kulimsukuma De Gea kuwa makini na kukaza Buti Mazoezini na kwenye Mechi.
Mourinho pia ameeleza uteuzi wa Kipa yupi atacheza Mechi zipi Msimu ujao utazingatia uzito wa Mechi na pia anataraji Kipa wa 3 Joel Pereira atajifunza mengi kutoka kwa De Gea na Romero.
WAPYA
Vile vile Mourinho amekiri ana nia ya kuongeza Wachezaji Wapya lakini amekiri ugumu wa Soko lenyewe.
Ameeleza: "Kutaja Majina ni ngumu kwangu kwani ni Wachezaji wa Klabu nyingine. Mameneja na Wamiliki wa Klabu nyingine hawapendi uzungumzie kununua Wachezaji wao. Hata mie sipendi uzungumzie Wachezaji wa Manchester United. Mie sifichi plani zangu..nilitaka Wachezaji Wanne ili Timu iwe na uwiano mzuri Kiwanjani."
Aliongeza: "Kwa sasa nakipenda Kikosi changu lakini bado nina matumaini ntaongeza wa 3 na labda wa 4!"
BALE HAJI
Wakati huo huo, Jose Mourinho amefuta kabisa kuwa Manchester United itatoa Ofa kumnunua Fowadi wa Real Madrid Gareth Bale katika kipindi hiki.
Kwa muda mrefu Man United imekuwa ikihusishwa na Bale na Mwaka 2013 nusura impate lakini Mchezaji huyo akasainiwa na Real Madrid kutoka Tottenham.
Lakini Mourinho amethibitisha kuwa, kama ilivyo kwa Cristiano Ronaldo, Bale si mlengwa wake.

No comments:
Post a Comment