SERIKALI YATANGAZA VIJANA ZAIDI YA 5,000 KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UANAGENZI NCHINI



 Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano) imetangaza rasmi orodha ya vijana 5,746 waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya uanagenzi kwa mwaka wa masomo 2025/2026. 

Mafunzo haya yanayofadhiliwa na serikali kwa 100%, yanalenga kuwapatia vijana ujuzi wa vitendo utakaowawezesha kujiajiri au kuajiriwa.

Akizungumza jijini Dodoma mnamo Januari 16, 2026, Waziri wa Nchi, Mhe. Deus Clement Sangu, amebainisha kuwa mafunzo hayo yatatolewa katika vyuo 47 nchini, yakihusisha fani mbalimbali za ufundi stadi kama vile ufundi magari, umeme, upishi, ushonaji, na ukataji wa madini.

Waziri Sangu amesisitiza kuwa mpango huu ni sehemu ya mikakati ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha nguvukazi ya Taifa na kuhakikisha vijana wa Kitanzania wanakuwa na ujuzi wa ushindani katika soko la ajira la ndani na nje ya nchi. 

Aidha, amevitaka vyuo husika kutoa usimamizi bora, huku akiwausia vijana waliochaguliwa kuzingatia nidhamu na masomo yao.

No comments