Miss
Tanzania mwaka 2001, Happiness Millen Magese ambaye anafanya kazi ya
uwanamitindo amebahatika kupata mtoto wake wa kwanza Julai 13 mwaka huu.
Millen
amewahi kumwaga machozi hadharani akielezea mateso yanayotokana na
tatizo aliloligundua kwake toka akiwa na umri wa miaka 13 la mirija yake
kuziba mwaka 2007.
Kuna
kipindi alikata tamaa mpaka akajiandaa kuondoa kizazi na hapo ni baada
ya kufanyiwa oparesheni zisizopungua 13 ambapo pamoja na hayo,
aliambiwa moja ya tiba ya tatizo hilo liitwalo ‘Endometriosis’ kwa
kizungu, ni kuzaa.
Baada
ya mateso yote usiku na mchana pamoja na kutumia gharama kubwa kwenye
matibabu South Africa na Marekani, hatimaye amefanikiwa kupata mtoto wa
kiume July 13 2017 Hospitalini New York Marekani na anaitwa Prince Kairo
Michael Magese.
No comments:
Post a Comment