MAKABIDHIANO YA BENDERA YA AFCON 2027 JIJINI RABAT
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda (wa pili kulia), akishiriki katika tukio la kihistoria la makabidhiano ya Bendera ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuashiria uenyeji wa michuano ya AFCON 2027.
Tukio hilo lililofanyika jijini Rabat, Morocco, lilihusisha makabidhiano kutoka kwa Makamu wa Rais wa CAF na Rais wa Shirikisho la Soka Morocco, Fouzi Lekjaa (katikati), kwenda kwa Mawaziri na Marais wa Mashirikisho ya Soka ya nchi za "Pamoja" (Tanzania, Kenya, na Uganda).
Wengine pichani ni Rais wa CAF, Patrice Motsepe (kushoto), akishuhudia hatua hiyo muhimu ambayo inathibitisha rasmi kuwa mataifa hayo matatu ya Afrika Mashariki yako tayari kuandaa mashindano makubwa zaidi ya soka barani Afrika.
(Picha na Mtandao)

Post a Comment