Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, July 22, 2017

RATIBA YA LA LIGA MSIMU WA 2017/18 HADHARANI, MABINGWA REAL KUANZA UGENINI, BARCELONA NYUMBANI DHIDI YA REAL BETIS


RATIBA ya Msimu Mpya wa La Liga wa 2017/18 imetoka na Mechi za kwanza kuchezwa Wikiendi ya kuanzia Agosti 18 ambapo Mabingwa Real Madrid wataanza utetezi wao Ugenini dhidi ya Deportivo La Coruna wakati Timu ya Pili Barcelona wataanza kwao Nou Camp kwa kucheza na Real Betis.

Vigogo hao Wawili watakutana uso kwa uso kwenye inayobatizwa El Clasico Wikiendi ya kuanzia Desemba 20 Uwanjani Santiago Bernabeu na kurudiana huko Nou Camp Wikiendi ya kuanzia Mei 6 kwenye Raundi ya 36 zikibaki Mechi 2 tu Ligi kumalizika.

Timu iliyomaliza Nafasi ya 3, Atletico Madrid, wao wataanza Kampeni Nyumbani kwao dhidi ya Girona FC wakati Sevilla wakicheza na Espanyol.

EL CLASICO: Real Madrid vs Barcelona (Wikiendi 20/12/17), Barcelona vs Real Madrid (Wikiendi 6/5/18)
Real Madrid v Barcelona - matchday 17
Barcelona v Real Madrid - matchday 26

Mechi za Ufunguzi kuchezwa Agosti 18-21
Athletic Bilbao v Getafe
Barcelona v Real Betis
Celta Vigo v Real Sociedad
Deportivo La Coruna v Real Madrid
Girona v Atletico Madrid
Leganes v Alaves
Malaga v Eibar
Sevilla v Espanyol
Valencia v Las Palmas
Villarreal v Levante

No comments:

Post a Comment