STRAIKA wa Spain wa Klabu ya Real Madrid Alvaro Morata sasa ananyemelea kutua moja kwa moja kwa Mabingwa wa England Chelsea baada ya kufuzu Vipimo vya Afya yake.
Wikiendi hii, Morata anatarajiwa kuruka kwenda Singapore kujiunga na Kikosi cha Chelsea ambacho kitakuwa huko kwa Ziara ya Mechi za Matayarisho kwa ajili ya Msimu Mpya.
Morata, mwenye Miaka 24, amehamia Chelsea kwa Ada ya Pauni Milioni 58 na alirejea tena Real mwanzoni mwa Msimu uliopita kutoka Juventus na kuifungia Real Bao 20 katika Mechi zake 43 akiisaidia Timu hiyo kutwaa Ubingwa wa La Liga na UEFA CHAMPIONZ LIGI. Staa huyo atakuwa Mchezaji wa Nne kusainiwa na Meneja Antonio Conte baada ya kuwanasa Willy Caballero, Antonio Rudiger na Tiemoue Bakayoko.
No comments:
Post a Comment