Monday, July 24, 2017
MAYANGA: BAHATI HAIKUWA UPANDE WETU
Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania, Salum Mayanga, amesema kwamba Taifa Stars haikuwa na bahati katika mchezo dhidi ya Amavubi ya Rwanda uliofanyika Uwanja wa Kigali ulioko kata ya Nyamirambo.
“Tumecheza vema, tulitafuta nafasi za kutosha. Tumeshambulia sana na kumiliki mpira. Lakini kila tulipojaribu kufunga, bahati haikuwa kwetu,” amesema Novatus mara baada ya mchezo huo.
Matokeo ya sare tasa ya jana yanawapa nafasi ya kusonga mbele Rwanda baada ya sare ya 1-1 katika mchezo uliofanyika Julai 15, mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Mchezo huo ni wa kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN) na sasa Rwanda itacheza na Uganda mwezi ujao.
Pamoja na kushindwa kusonge mbele, Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti, imeendeleza rekodi yake ya kutopoteza mechi baada ya kucheza mechi 11 za kimataifa na kushinda mitano; kutoka sare mitano na kufungwa mmoja wa nusu fainali za Cosafa.
……………………………………………………………..………………………….
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment