SAKATA la
mkataba wa mshambuliaji wa Kagera Sugar Mbaraka Yusuph ambaye amesajiliwa na
Azam FC msimu huu limeingia katika sura mpya baada ya mchezaji huyo kwenda katika
Ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuchukua nakala ya mkataba wake wa
zamani na kupewa mikataba miwili tofauti.
Akizungumza Meneja Mkuu wa Azam FC, Abdul Mohamed alisema kabla ya kuingia
makubaliano ya kusaini mkataba na Mbaraka walijiridhisha kuwa hana mkataba na
Kagera lakini wameshangaa baada ya kwenda TFF na kupewa mikataba miwili tofauti
“Sisi Azam FC tulikuwa na nakala halisi ambayo
iliwasilishwa TFF kwenye usajili ulikwish lakini tulimwambia Mbaraka akachukue
nakala yake TFF, ajabu amepatiwa nakala mbili tofauti,”.
“Nakala moja
inaonyesha mkataba uliosainiwa ni wa mwaka mmoja ambao ulisainiwa Juni 20, 2016
na mwingine unaonyesha ni wa miaka mitatu ambao umesainiwa Agosti 10, 2016,”
alisema Abdul
Pia Abdul
alisema ukiacha tofauti ya miezi mitatu ya kusainiwa mikataba hii, lakini hata
kiwango cha usajili ni tofauti mno kwani mkataba wa miaka mitatu hauna saini ya
mchezaji, wala muhuri wa Kagera Sugar na jina la mchezaji kwenye sehemu ya
kusaini halijaandikwa.
Aidha Abdul
alisema wataiweka hadharani mikataba
hiyo endapo mchezaji Mbaraka ataridhia ili familia ya soka ione mikataba
yote miwili na kisha tarataibu nyingine zifuate kwani kuna uhuni mwingi ambao
unafanywa kwenye baadhi ya mambo, hasa masuala ya mikataba ya wachezaji.
”Sisi Azam
tunataka kulimaliza tatizo hili. Na kwa hili tutatumia wanasheria wetu
kuwafikisha mahakamani wote walioshiriki kufoji mkataba wa Mbaraka ili kujenga
precedent nzuri huko mbele,” alisema Abdul
Abdul
aliwataka uongozi wa Kagera Sugar kukanusha au kuthibitisha juu ya mikataba hii
ili hatua stahiki ziweze kufuatwa kwani suala la kufoji mikataba ya wachezaji
ni uhuni ambao haupaswi kuachwa kuendelea kwenye mpira.
No comments:
Post a Comment