Serikali
imesema ni marufuku kwa shule ambayo itakuwa haina viwanja vya michezo kupatiwa
kibali cha kufungua shule ikiwa ni utekelezaji wa Sheria ya Elimu namba 25 ya
mwaka 1978.
Akizungumza
wakati wa Ufunguzi wa Masindano ya kwashule za msingi nchini UMITASHUMTA mkoani
Mwanza, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(OR-TAMISEMO) Mh. George Simbachawene, amemuagiza Kamishna wa Elimu nchini,
kutozipatia vibali shule zinazo hitaji kufunguliwa endapo zitakuwa hazina
viwanja vya michezo.
Simbachawene,
amesema kutokana na sheria ya Elimu namba 25 ya mwaka 1978, ambayo inataka kila
shule inapofunguliwa lazima iwe na viwanja visivyo pungua vitano hivyo nilazima
hili lizingatiwe, “nichukue nafasi hii kumuagiza
kamishna wa Elimu kuanzia sasa asisajili shule yeyote ile ambayo itakuwa haina
Viwanja vya michezo, kwani bila kufanya hivyo azma yetu yakuinua michezo nchini
haiwezi kutimia.”
Mbali na
kutoa maagizo hayo waziri Simbachawene, ameziagiza pia halmashauri na wilaya
kote nchini kutenga sehemu ya mapato yao ya ndani kwaajili ya kitengo cha
michezo, huku akizihimiza kuweka katika bajeti ijayo ya serikali fedha kwenye
vifungu vinavyo husiana na michezo na kuonya kuwa endapo Halmashauri itashindwa
kufanya hivyo basi yeye kama waziri mwenye dhamana hatakubali ipite.
Amesema
Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015 sehemu ya (61) inatambua suala la
Michezo lakini pia Sera ya Elimu ya Mwaka 1995, hivyo kama Serikali lazima
waweke kipaumbele katika suala zima la michezo.
Ameongeza
kuwa, Msingi wa Michezo nchini ni michezo ya UMITASHUMTA NA UMISETA ndio Dira
ya timu zetu za Taifa, “Tukiwaandaa vijana wetu vizuri na kutokana kaulimbiu
hii ya masula ya viwanda, hatuna wasiwasi kuwa hawa ndio viwanda vyenyewe,
mchezaji mmoja aliyefikia viwango vya kimataifa huweza kugharamia hata bajeti
ya nchi” alisema Simbachawene.
Katika hatua
nyingine Simbachawene, amewaagiza makatibu Tawala kote nchini, kusimamia suala
la taaluma na michezo, amesema hakuna taaluma bila Michezo na Hakuna michezo
bila Taaluma kwa mantiki hiyo lazima nidhamu ya hali ya juu iongezwe miongoni
mwa vijana na wanamichezo kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment