MBIO za
kuwania uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), zimezidi kushika kasi
baada ya Ofisa wa juu Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Shija Richard kujitosa
kuwania urais wa shirikisho hilo.
Shija
ambaye ni Meneja ndani ya Mamlaka ya Mapato Tanzania, amechukua fomu hiyo leo
Jumatatu katika ofisi za TFF Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, ingawa
hakuzungumza lolote kwa maelezo kuwa muda wa kampeni bado.
“Ni kweli
nimechukua fomu kuwania urais wa TFF, wengi mtataka kujua mengi kuhusu mimi na
kwa nini nimejitosa katika nafasi hii, tuvute subira wakati wa kampeni ukifika
nitazungumza, ila kwa leo itoshe kuuthibitishia umma kwamba nimechukua fomu ya
urais,” alisema Shija.
Mgombea huyo
ana Shahada ya Uzamili katika masuala ya Sheria za Kodi na Utawala kutoka Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam, pia ana Stashahada ya Uzamili ya Usimamizi wa Fedha
kutoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Dar es Salaam na Stashahada ya Juu ya
Uhasibu kutoka Chuo Kikuu cha Uhasibu Arusha (IAA).
Pia Shija
amehudhuria mafunzo mbalimbali ya uandishi wa habari na ameandikia magazeti
mbalimbali hapa nchini kuanzia mwaka 1997.
Mgombea
huyo aliwahi kuitumikia Taasisi ya Kuzuia na Kupambaana na Rushwa (TAKUKURU)
kabla ya kujiunga na Mamlaka ya Mapato Tanzania. Kwa sasa ni Mhazini Mkuu
wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (TASWA), akiwa pia amepata
kuongoza klabu mbalimbali za mpira wa miguu kwa ngazi tofauti.
Mwaka 2008
alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Muda ya Chama cha Soka wilayani Chato
(CDFA), ambapo alisimamia usajili wa chama hicho kuelekea kwenye uchaguzi ambao
hata hivyo hakugombea.
Pia Shija amepata kuwa Katibu Mkuu wa Klabu ya Michezo
ya Bukoba Veteran iliyopo mkoani Kagera.
Wakati huo huo mchezaji wa
zamani wa Yanga na Taifa Stars Ally Mayay ‘Tembele’ jana alichukua fomu ya
kugombea Urais wa Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF).
Mayay ambaye
aliambatana na mchezaji mwingine wa zamani Mtemi Ramadhani walifika TFF kwa
ajili ya kuchukua fomu, Mtemi anawania nafasi ya makamu wa Rais wa TFF.
Wawili hao
walisindikizwa na wachezaji wa zamani wakiongozwa na kocha Jamhuri Kiwelu
‘Julio’, Duwa Said, Salvatory Edward,
Jembe Ulaya, Khalid Abeid na wachezaji wengine.
Msafara wa
Mayay ulikuwa umebeba mabango yenye ujumbe unaosomeka Bring back our ball
“Turudishieni mpira wetu.”
No comments:
Post a Comment