KIUNGO mshambuliaji wa Azam FC, Farid Mussa anatarajia kuondoka nchini kesho
usiku kuelekea Hispania baada ya kutumiwa tiketi ya ndege na klabu ya Tenerife
inayoshiriki ligi daraja la pili
Akizungumza na wandishi wa habari jana, Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffa Idd alisema Farid ataondoka saa 5 usiku kwa ndege ya KLM ambapo atapitia Amsterdam, Barcelona hadi kufika Tenerife na kujiunga na timu hiyo kwa mkopo.

"Kesho saa 5 usiku Farid ataondoka kwenda Hispania kwa ndege
ya KLM kujiunga na timu ya Tenerife inayoshiriki ligi daraja la pili, tayari
ametumiwa tiketi kwa ajili ya safari hiyo na sisi Azam tunamtakia kila la kheri
katika maisha mapya ya soka" alisema Jaffa huku akiwaonesha wandishi
tiketi hiyo.
Farid anakwenda Tenerife kwa mkopo hivyo Azam FC watakuwa wanamlipa stahiki zote ikiwemo mshahara kwa mujibu wa mkataba walioingia na klabu hiyo.
Awali Tenerife walitaka kumsajili winga huyo kwa mkataba wa moja kwa moja baada ya kufaulu majaribio lakini dau ambalo walitaka kutoa lilikataliwa na Azam kwakuwa lilikuwa dogo na baadae walikubaliana kumchukua kwa mkopo.

Kuondoka kwa Farid kunaweza kufungua milango kwa wachezaji wengine wa
Tanzania kwavile atautangaza vyema mpira wa nchi hii.
No comments:
Post a Comment