MENEJA wa Simba, Musa Mgosi amemtumia
salamu za pongezi, beki wao wa kimataifa Juuko Murshid baada ya mke wake
kujifungua watoto mapacha watatu juzi.
Akizungumza na gazeti hili, Mgosi
alisema ni jambo la heri na kumshukuru Mungu kwa kumjaalia mwezetu kupata
watoto mapacha na wanamwomba Mungu awape afya tele.
“Juuko yupo kwenye timu ya Taifa ya
Uganda lakini tumepokea taarifa hizo njema kwa furaha hivyo tunampongeza sana,”
alisema Mgosi
Kwa mujibu wa Mgosi mke wa Juuko anaitwa
Ruth na anaendelea vema yeye pamoja na watoto.
Juuko hajajiunga na Simba katika
mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara kwa sababu yupo kwenye kambi ya timu ya Taifa
ya Uganda ‘The Cranes’ kujiandaa na mashindano ya Afrika yatakayofanyika Gabon.
No comments:
Post a Comment