MSHAMBULIAJI wa Mbeya City, Zahoro Pazzi anatarajia kucheza mchezo wake
wa kwanza akiwa na timu hiyo Desemba 31, dhidi ya Mbao FC, utakaochezwa kwenye
Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Zahoro ambaye alisajiliwa na timu hiyo kwenye dirisha dogo amesema
anamshukuru Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, Jamal Malinzi kwani amepata
ITC yake iliyokuwa ikishikiliwa na FC Lupopo ya DR Congo kwa miaka miwili sasa.
“Namshukuru Rais Malinzi kwa kusikia kilio changu kwani niliandika kwenye
mtandao wa kijamii kuhusu ITC yangu iliyokuwa inashikiliwa na FC Lupopo kinyume
na utaratibu na alipoisoma alinitafuta akaniahidi ndani ya siku saba nitaipata,
nashukuru nimeipata,” alisema Zahoro.
Pia Zahoro amewataka wachezaji wenzake endapo wana tatizo wasiogope
kulifikisha ngazi za juu kwani watapata msaada kwa wakati.
“Mimi ningeogopa naamini hadi leo nisingekuwa nimepata ITC yangu lakini baada ya kumwomba Rais Malinzi msaada alikutana na mimi nikamweleza sakata lote na kuahidi kulishughulikia ndani ya siku saba na kweli nimepata,” alisema Zahoro.
Zahoro hajawahi kucheza FC Lupopo lakini ITC yake ilitolewa kwa uongozi wa timu hiyo na mmoja wa viongozi ndani ya shirikisho jambo ambalo Zahoro anasema ilikuwa kinyume kwani hawakufikia makubaliano ya kwenda kucheza huko.

No comments:
Post a Comment