Mapema Mwezi huu, Arsenal iliivamia Leicester na kutoa Ofa ya Pauni Milioni 20 ambayo ndiyo imo kwenye Mkataba wa Vardy akitakiwa na Klabu nyingine na kila dalili zilikuwepo kwamba atahamia Emirates.
Lakini Vardy
mwenyewe akasita kutoa uamuzi wa haraka na Wiki iliyopita Meneja wa
Arsenal, Arsene Wenger, akanyoosha Mikono juu na kuungama kuwa Straika
huyo aliefunga Bao 24 na kuipa Ubingwa Leicester atabakia Leicester.
Leo Leo Leicester imetoa taarifa rasmi kuthibitisha kuwa Vardy, ambae yupo France na Kikosi cha England kinachocheza EURO 2016, atabaki King Power Stadium kuisaidia Timu yake kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI kwa mara ya kwanza Msimu ujao.
Taarifa hiyo imesema wametoa pande zote mbili zinaafiki tangazo lao ili kuondoa utata kuhusu hatima ya Vardy.
Nae Straika wa France Antoine amesaini Dili mpya na Atletico Madrid ambayo itamweka hadi 2021.
Griezmann amekuwa akitangazwa sana kuhamia Klabu za Ligi Kuu England huku mwenyewe akikiri ana furaha kubakia Spain ambako amemaliza Misimu yake Miwili na Atletico akiwa ndie Mfungaji Bora wao.
Magoli ya Griezmann yameisaidia Atletico kumaliza La Liga mara mbili wakiwa Washindi wa Tatu na pia alipiga Bao 7 kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI ambako walitinga Fainali na kutolewa na Real Madrid kwa Mikwaju ya Penati Tano Tano.

No comments:
Post a Comment