Timu ya soka ya Vijana
ya Shelisheli, imeingia Dar es Salaam, Tanzania usiku wa kuamkia leo Juni 24,
2016 saa 7.45 usiku wa kuamkia leo Ijumaa Juni 24, 2016, kwa ajili ya mchezo
dhidi ya timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti
Boys’ utakaofanyika Juni 26, 2016 kuanzia saa 10.00 jioni kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Timu hiyo imeingia
wachezaji na pamoja na viongozi 25 ka ujumla wake na imefikia hoteli ya
Southern Sun iliyoko katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Waamuzi wanne kutoka
Ethiopia, ndio watakaochezesha mchezo wa kimataifa kati ya timu ya Taifa ya
Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ na Shelisheli
utakaofanyika Juni 26, 2016 kuanzia saa 10.00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.
Mchezo huo ni wa
kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa kwa vijana wenye umri wa
chini ya miaka 17. Waamuzi hao ni Belay Tadesse Asserese ambaye ni mwamuzi wa
kati wakati wasaidizi wake ni Tigle Gizaw Belachew upande wa kulia na Kinfe
Yilma Kinfe upande wa kushoto huku mwamuzi wa akiba atakuwa Lemma Nigussie.
Kamishna wa mchezo huo atakuwa ni Bester Kalombo.
Serengeti Boys
ilikuwa kambini tangu Juni 14, 2016 kujiandaa na mchezo huo wa kufuzu fainali
za Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya vijana wenzao wa Shelisheli
utakaofanyika Juni 26, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Mchezo wa marudiano kati ya Serengeti Boys na Shelisheli utachezwa Julai 2,
2016 huko Shelisheli.
Katika kuajindaa na
mchezo huo, Serengeti Boys ilifanya ziara India ambako walishiriki mashindano
ya vijana ya Kimataifa yanayotambuliwa na FIFA (AIFF International Youth
Tournament 2016) kabla ya kurudi na rekodi ya kupigiwa mfano si tu katika
Tanzania na kwa nchi za Afrika Mashariki.
No comments:
Post a Comment