TIMU ya soka ya Taifa ya soka ya wanawake ‘Twiga Stars’ leo imejikuta katika wakati mgumu baada ya kufungwa mabao 2-1 na Zimbabwe ‘Mighty Warriors’ katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika.
Zimbabwe, wanayotoka wachezaji nyota wa Yanga, kiungo Thabani Kamusoko
na mshambuliaji Donald Ngoma, pamoja na kiungo wa Simba, Justice Majabvi, walionesha
umahiri mkubwa na kuonekana kana kwamba wao ndiyo wenyeji.
Kocha Mkuu wa Twiga Stars, Nasra
Juma itabidi afanye kazi ya ziada kuwanoa vijana wake kuhakikisha nao wanaenda
kushinda katika mchezo wa marudiano.
Mechi ya marudiano itachezwa Zimbabwe
Machi 18 ambapo timu itakayovuka raundi hiyo itamenyana na mshindi kati ya
Zambia na Namibia. Fainali za michuano hiyo zimepangwa kufanyika Cameroon
baadaye mwaka huu.
No comments:
Post a Comment