Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania bara inatarajiwa kuendelea mwishoni mwa wiki
hii kwa michezo sita kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini, huku
michezo mitatu ikichezwa siku ya jumamosi na michezo mingine mitatu
ikichezwa siu ya jumapili.
Jumamosi
katika Uwanja wa Sokoine wapinzani wa jiji la Mbeya, Prisons FC watakua
wenyeji wa wagonga nyundo Mbeya City mchezo utaochezwa majira ya saa 10
kamili kwa saa za Afrika mashariki na Kati.
Katika
Uwanja wa Nangwanda Sijaona wenyeji timu ya Ndanda SC watawakaribisha
wakata miwa wa Kagera Sugar, huku jijini Tanga Mgambo Shooting wakiwa
wenyeji wa maafande wa JKT Ruvu mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa
Mkwakwani.
Jumapili
katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaa, Simba SC watawakaribisha
Azam FC, mchezo ambao unatabiriwa kuwa na upinzani mkali kusaka nafasi
ya pili ili mwakani kuweza kuwakilisha Tanzania katika michuano ya Kombe
la Shirikisho barani Afrika.
Jijini
Tanga wagosi wa kaya Coastal Union watawakaribisha timu ya Stand United
kutoka mjini Shinyanga, mchezo utakaochezwa kwenye uwanja wa Mkwakwani,
huku kwenye Uwanja wa Manungu mjini Morogoro wenyeji Mtibwa Sugar
wakiwakaribisha maafande wa Ruvu Shooting.
No comments:
Post a Comment