Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini - TFF, Jamal Malinzi amewatakia
kila la kheri Wawakilishi pekee wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho
Barani Afrika (CC) timuYoung Africans katika mchezo wake wa marudiano
dhidi ya timu ya Etoile du Sahel utakaochezwa kesho nchini Tunisia.
Katika
salamu zake Malinzi amesema ,Young Africans wakiwa ndio timu
wawakilishi pekee wa Tanzania na Afrika Mashariki katika michuano ya
kimataifa barani Afrika wanapaswa kupambana kuhakikisha wanasonga mbele
katia hatua inayofuata.
Katika
mchezo wa awali uliofanyika wiki mbili zilizopita jijini Dar es salaam,
Young Africans ilitoka sare ya bao 1- 1 na Etoile du Sahel, na mshindi
wa jumla kwa mchezo wa huo, atacheza hatua ya mtoano (Play-off) dhidi ya
timu zitakazokuwa zimetolewa kwenye Ligi ya Mabingwa (CL) kuwania
kufuzu kwa hatua ya makundi.
Mchezo
huo wa marudiano utapigwa kesho jumamosi katika dimba la Olympique de
Sousse katika mji wa Sousse kuanzia majra ya saa 3 kamili usiku kwa saa
za Afrika Mashariki na Kati.
No comments:
Post a Comment