HUYU NDIO RAIS WA BURUNDI NKURUNIZA. AJILIWAZA NA SOKA WAKATI ................
Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza ameonekana akicheza mpira pamoja na
marafiki zake mjini Bujumbura licha ya mgogora wa kisiasa nchini mwake.
Hii leo habari kutoka Burundi zinasema kuwa mtu mmoja amepigwa risasi na kuuawa katika mji mkuu wa Bujumbura.
Walioshuhudia wanasema kuwa polisi walimpiga mwandamanaji huyo risasi mgongoni wakiwa katika eneo la Musaga linalotazamwa kama ngome ya upinzani.
Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza, amewaomba zaidi ya raia laki moja na hamsini waliokimbia ghasia nchini humo katika majuma kadhaa yaliyopita, warejee nyumbani.
Anasema kuwa hakuna mtu yeyote anayetaka kufufua taharuki ya kikabila.
Post a Comment